...

Hospitali ya kibinafsi ya Hopekins Yaanda Michezo ya riadha,Omanyala ahusishwa.

Dishon Amanya – Bungoma

Bingwa wa mita 100 Barani Afrika Ferdinand Omanyala anapania kufungua kambi za kukuza talanta za wanariadha wa mbio hizo kila eneo hapa nchini Kenya ili kuhakikisha utafutaji wa wanariadha zaidi watakaochukua nafasi yake akistaafu.

Omanyala Akizungumza wakati wa mbio za Hopkins Run Wellness Awamu ya Kwanza mjini Bungoma,amesema kwamba nchini Kenya kuna talanta nyingi mashinani na iwapo wataziangazia basi Kenya itashinda katika kila mchezo duniani.

Amesema kuwa atakuwa akiwachagua watoto wa shule za msingi na kuwakuza hadi kumaliza kidato cha nne kabla ya kujiunga na Omanyala Foundation Camp Jijini Nairobi.

Viongozi waliohudhuria mbio hizo wakiongozwa na Gavana Kenneth Lusaka, Mwenyekiti aa kamati ya Spoti Bungeni Dan Wanyama na Viongozi wengine wamesema kuwa hatua hiyo kando na kutambua talanta inasaidia mazoezi ya kimwili.

Kinyang’anyiro hicho kilijumuisha uendeshaji wa Baiskeli, Mita 100 ,Skating mbio za Kilomita 8 ,Wakimbiaji walioshiriki michuano hiyo wakipongeza na kutaka kuwepo kwa michezo kama hiyo mara kwa mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Seraphinite AcceleratorOptimized by Seraphinite Accelerator
Turns on site high speed to be attractive for people and search engines.