Dishon Amanya – Bungoma
Eneo la Mlima Elgon kutoka kaunti ya Bungoma ni maarufu katika shughuli za ukulima, lakini licha ya kuwa kitovu cha uzalishaji vyakula wakaazi wanataabika sana kundeleza biashara zao kutokana na miundo misingi mbovu ikiwemo barabara. Jumatatu ya tarehe tano mwezi Agosti, wenyeji wa Chebyuk kutoka eneo Bunge la Mlima Elgon waliandamana hadi katika Afisi inayosimamia ujenzi wa barabara ya KERRA, mjini Bungoma wakidai kusahaulika kwa miaka na mikaka kukarabatiwa kwa barabara ya Chebyuk-Cheptono, huku wakidai kuwa pesa zilizotengewa barabara hiyo zimekuwa zikielekezwa katika ukarabati wa barabara zingine. “Kila mwaka huwa tunaona barabara zingine zikikarabaitiwa ilhali hii yetu ya Chebyuk imekuwa ikisahauika licha ya serikali kuwekeza hela za ukarakabati katika bajeti,” Chrispine Kipsang, mkaazi wa Chebyuk aeleza. Aidha, kulingana nao wamedokeza kuwa kuna barua inayosambaa wakidai wanakisia inasambazwa na mbunge wa eneo hilo kuwa barabara hiyo haipo katika ramani ya kufanyiwa ukarabati,
Kulingana na kauli yake Chrispine, mnamo mwaka wa 2019 wakati Fred Matiang’i alizuru eneo hilo, shilingi milioni 40 iitengwa kwa minajili ya usalama wa barabara hiyo lakini hilo halikufanyika kamwe. Pesa ambayo ilitengewa barabara hiyo ni milioni 5 ambayo ilipaswa kukarabati barabara hiyo yenye kilomita 17 lakini hilo limekuwa ndoto kwa wenyeji hawa tangu mwaka wa 1999 ambapo wamekuwa wakipigania kupata barabara nzuri” Akina mama wamekuwa wakipoteza maisha wanapokimbizwa kupata huduma za afya hospitalini kutokana na barabara mbovu, kufika katika vituo vya afya imekuwa ni shida,” Carol Kokus mkaazi wa eneo hilo anaeleza. Licha ya kutopata haki wakaazi wamedokeza kuwa hawatalegeza kamba hadi pale ambapo kilio chao kitasikika, wanadai mashirika husika kuingilia katika ikiwemo EACC ili kufanya uchunguzi wa iwapo kulikuwa na matumizi mabaya ya fedha za barabara.Tukio hili linafanyika wakati ambapo kaunti ya Bungoma ikimulikwa vikali kwa matumizi mabaya ya pesa za umma.